MSANII mkongwe wa filamu Bongo Issa Musa ‘Cloud’ amekana tuhuma zinazosambazwa mtandaoni kuwa alimfitini muigizaji mwenzake, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ ili kumzuia asisafiri kuelekea Uingereza miezi michache iliyopita.
“Mimi sikumfitini Frank, yule mtu alinifuata mwenyewe kwa makubaliano ya mdomo kuwa nikacheze filamu, sikuwa peke yangu, tuliongozana na kina Monalisa na Riyama, tatizo ni la huyo aliyenipeleka kule, nilifanya mambo kwa mazoea na ndiyo sababu anaamua kusambaza uongo dhidi yangu,” alisema mkongwe huyo wakati akizungumza na Global Tv.
Aliwasihi wasanii wenzake nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wahakikishe wanaingia mikataba ya maandishi ili wawe na ushahidi wakati waliokubaliana nao kazi wanapoleta ujanjaujanja kama ilivyomtokea yeye katika safari hiyo ya Uingereza ambayo sasa inamletea uadui na Frank.