Wednesday, October 8, 2014

HUYU NDIYE ANDREW MBUGUA MWANAUME ALIYEBADILI JINSIA KUWA MWANAMKE, KWA SASA ANAITWA BI; AUDREY MBUGUA

Audrey amekuwa akitaka baraza la mitihani kubadili jina lake na utambulisho wake wa kijinsia
Mwanaume aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke na kutaka jina lake kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi yake dhidi ya baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.
Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi la serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.
'Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo,'' alisema jaji.
Jaji alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu kuwaheshimu wengine kama ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo mengi ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey kuhisi kuwa sawa anapaswa kukubalika kama alivyo na kumyima haki hiyo ya kubadilisha jina lake katika chati chake itakuwa ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwa mteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.