Wednesday, October 8, 2014

BARCELONA KUTIMULIWA LA LIGA IWAPO KATALUNYA ITAJITENGA HISPANIA

KLABU ya Barcelona haitaruhusiwa kucheza La Liga ikiwa Katulonya itajitenga kutoka Hispania, Mkuu wa ligi ya nchi hiyo, Javier Tebas amesema hayo juu ya uwezekano wa mgawanyiko wa taifa hilo mwezi ujao.
Tebas amefafanua kwamba sheria za michezo za nchi hiyo zinaruhusu nchi moja tu ambayo si sehemu ya Hispania - Andorra - kushiriki ligi hiyo au mashindano mengine, na FC Andorra tayari inacheza katika mfumo wa za Hispania.
Huku La Liga tayari ikionekana kuwa na timu mbili zinazochuana vikali kwenye vita ya mataji (pamoja na Atletico Madrid kushinda taji msimu uliopita kuzima utawala wa Real na Barca kwa misimu tisa) kuwapoteza vigogo hao wa Katalunya litakuwa pigo kubwa kwa soka ya Hispania.

Vigogo wa Hispania, Barcelona moja kwa moja watakuwa wamejiondoa La Liga ikiwa Katalunya litakuwa taifa huru

"Ikiwa Katalunya litakuwa taifa huru, kwa kuzingatia Sheria za Michezo Hispania, kwamba Barcelona haitaruhusiwa kucheza," Tebas, rais wa LFP, amewaambia Waandishi wa Habari mjini Barcelona.
"Yatahitajika mabadilika katika sheri a zilizowekwa na Bunge la Hispania. Wazi, iwapo itatokea litakuwa pigo kubwa katika soka ya Hispania kuwap[oteza Barca.
"Sipati picha LFP bila Barca. Kwa namna hiyo hiyo siwezi kupata picha Katalunya bila Hispania, Siioni La Liga bila Barca. Pia ikiwa itatokea hivyo, utaiitaje hiyo ligi: Ligi ya Hispania au Ligi ya Iberia?'
Sababu ambazo zimeipa Andorra fursa ya kucheza ligi ya Hispania, nchi ndogo kwenye milima ya Pyrenees inayozitenganisha Hispania na Ufaransa- zinaweza kutumika pia kuzifanya klabu za Katalunya ziendelee kushiriki.
Barcelona, with superstars like Lionel Messi in their team, could be made to play in the Catalan League
Barcelona, ikiwa na nyota kama Lionel Messi katika timu yao, watabaki kucheza Ligi ya Katalunya
Xavi na Gerard Pique ni miongoni mwa wachezaji wa Barca waliojitokeza kuunga mkono kung a mkono kujitenga kwa Katalunya. Serikali ya Katalunya itaamua Oktoba 15 juu ya mustakabali wa nchi yao.