Sunday, October 12, 2014

KITOWEO' CHA SUAREZ CHAPIGA 'HAT TRICK' ITALIA IKISHINDA 2-1 KUFUZU EURO

YULE mchezaji aliyeng'atwa meno na Luis Suarez kwenye Kombe la Dunia, Giorgio Chiellini usiku wa jana amefunga mabao yote matatu peke yake, Italia ikiilaza Azerbaijan 2-1 katika mchezo wa Kundi H kufuzu Euro The Azzurri wakiendelea vizuri chini ya kocha mpya, Antonio Conte.
Azerbaijan 'walipaki basi' wakicheza na walinzi 10 na Italia ikapata tabu sana kuupenya ukuta wao hadi Chiellini alipotumia makos a ya kipa kuipa Azzurri bao la kuongoza dakika ya 44.
Chiellini akajifunga kuisawazishia Azerbaijan dakika ya 76 katika harakati kuokoa mpira wa kona- lakini bahati nzuri akasahihisha makos a yake kwa kuifungia Italia bao la ushindi dakika ya 82.
katika mechi nyingine za Kundi H, Croatia imeifunga 1-0 Bulgaria bao pekee la Nikolay Bodurov la kujifunga dakika ya 36 na Norway imeifunga 3-0 Malta, mabao ya Moeller Daehli dakika ya 22 na Joshua King dakika ya 26 na 49.  

Giorgio Chiellini amefunga mabao yote matatu Italia ikiichapa Azerbaijan 2-1