Thursday, October 16, 2014

MAJANGA. ROSE MHANDO NA HII TENA ADAIWA KUTAPELI TENA

utapeli wa shilingi milioni mbili.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Rose
Muhando.
Muandaaji wa shoo hiyo, Ibrahim alidai kuwa
Rose alitumiwa kiasi hicho cha pesa kama
sehemu ya malipo ya kazi hiyo iliyokuwa
ifanyike Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa
Hoteli ya Landmark uliopo Ubungo, jijini Dar
lakini hakutokea.
“Huu ni utapeli wa hali ya juu, maana alipewa
pesa yote ya shoo, cha kushangaza hakutoa
taarifa yoyote ya dharura, simu akipigiwa
hapokei na wala meseji hajibu,” alisema
Ibrahim.
Rose alipopigiwa simu ili kujua madai hayo
kama yana ukweli, simu yake iliita bila ya
kupokelewa hivyo akatumiwa meseji ambayo
nayo ilionesha kumfikia lakini hakujibu
chochote.
Hivi karibuni, Rose alidaiwa kuingia mitini na
shilingi milioni moja aliyopewa kama malipo ya
kutumbuiza katika uzinduzi wa albamu ya
mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.