Monday, October 20, 2014

MISS TZ 2014 AKIMBILIA KANISANI

Ziba masikio, fanya yako! Wakati watu wakichonga juu ya sakata la madai ya kuwa na mtoto na utata juu ya umri wake, Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu anadaiwa kukimbilia kanisani.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu.
Habari za uhakika zilidai kwamba, baada ya kutwaa taji hilo hivi karibuni na kuibua sintofahamu, mrembo huyo alikimbilia kwenye Kanisa la Ufunuo kwa Nabii Yaspi Bendera lilipo Yombo-Buza jijini Dar kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoto yake ya kuwa Miss Tanzania.
Ilidaiwa kwamba, Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke kwa leseni ya CCM, Abbas Zuberi Mtemvu, akiongozana na mama yake, walikwenda kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wema aliomtendea Mungu.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu aliopotangazwa mshindi.
“Watu wanaendelea kumsema  mtoto wa mwenzao huku yeye anamshukuru Mungu kwa sababu hata kabla hajatwaa taji hilo alikuwa akisali hapa hivyo Mungu amepokea maombi yake na si vinginevyo kama watu wanavyomsimanga,” alisema   muumini mmoja wa kanisa hilo.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nabii Yaspi ili kupata uhakika wa mrembo huyo kutinga kanisani kwake ambapo alikiri ni kweli alikwenda kanisani kwake na ameshampigia maombi kwa Mungu hivyo atanyakua Taji la Miss World mwaka huu.
Nabii Yaspi Bendera wa Kanisa la Ufunuo lilipo Yombo-Buza jijini Dar.
Sitti alishiriki shindano hilo tangu ngazi ya vitongoji na kutwaa Taji la Miss Temeke kabla ya kuibuka kidedea kwenye Miss Tanzania linalofukuta ambapo kesho (Jumanne), mkurugenzi wa shindano hilo, Hashim Lundenga anatarajiwa kutoa tamko rasmi.