Monday, October 27, 2014

RIYAMA, ROSE WAMPA WAKATI MGUMU JB..WAMKOMALIA AKATE MAUNO HADHARANI

OHOOOO! Wasanii wa filamu Bongo, Riyama Ally na Rose Ndauka wamemkomalia msanii mwenzao, Jacob Steven ‘JB’ akate mauno mbele ya hadhara kitendo ambacho kilimshinda msanii huyo mwenye ‘weight’ ya kutosha.
Wasanii wa filamu Bongo, Riyama Ally na Rose Ndauka wakimtaka msanii mwenzao, Jacob Steven ‘JB’ akate mauno mbele ya hadhara.
Tukio hilo lilijiri mwishoni wa wiki iliyopita maeneo ya Mwananyamala jijini Dar kulipokuwa na sherehe ya bethidei ya mtangazaji wa kituo cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ ambapo wasanii hao walimkomalia JB atoe shoo akawagomea kwa kisingizio cha kuokoka.
Rose Ndauka akikata mauno 'JB', huku Riyama akimkomalia 'JB' acheze. 
“Jamani sasa mbona mnanilazimisha hivi, nyie watoto acheni kunikomalia au mmeshalewa? Mimi siwezi kucheza bwana sasa hivi nimeokoka,”alisema JB jambo ambalo liliwafanya wanadada hao kuishiwa pozi pamoja na kumshawishi kwa muda mrefu