kuhusu chanzo cha ugomvi wao lakini pointi ya msingi ni kupishana kauli kibinadamu kama watu wengine wanavyoweza kutofautiana na kupatana.
Kwa upande wao suala la kupatana limekuwa zito, ugomvi wao haufiki tamati hukukila kukicha ni malumbano ambayo yanawagawa mashabiki.
Makundi hayo ndiyo yamekuwa chachu kubwa ya bifu lao na kuzidisha mapambano kati ya mastaa hawa ambao naamini wanapendana sana, sitaki kuamini kabisa kama Wema hampendi Kajala, na sitaamini kama Kajala hampendi Wema.
“Mimi nilikuwa napenda sana kukuangalia wewe na siyo timu zinazotuzunguka zinazidi kututia chumvi tugombane, nakupenda na ninajua ni rafiki mwema kwangu lakini unasikiliza sana maneno ya watu,” ni maneno ya Kajala niliyosikia akimwambia Wema.
“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
Nathubutu kusema kwamba ugomvi wa mastaa hawa mara nyingi unachagizwa na mitandao ya kijamii. Hizi zinazojiita Team Wema na Team Kajala ndiyo tatizo kubwa.Nasema ni tatizo kwa sababu hata ukiangalia kwa makini, kipindi cha nyuma mastaa hawa walipokuwa wanaanzisha urafiki wao, timu hizo hazikuwepo ndiyo maana waliweza kudumu.
Kwa nini wanakubali kutawaliwa na hizi Team? Kwa nini waruhusu maisha yao ya kila siku yaingiliwe uhuru wao wa kufanya mambo yao? Si sawa!
Mimi naamini kabisa kama mastaa hawa wangekuwa na ugomvi wao bila hizi Team kuingilia kati wangeweza kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao mapema sana lakini tatizo kuna watu wa pembeni wenye kuzoa maneno huku na kupeleka kule.
Kwa jinsi ninavyoona mimi, hizi Team zikiendelea hivi na kwa mastaa wengine, ipo siku watasababisha hata mauaji kwa jambo ambalo halina kichwa wala miguu. Niwasihi Kajala na Wema wasijisahau kuwa wao ni biashara, mashabiki wengi wanapenda kuona kazi zao, wangeweka tofauti zao pembeni wafanye kazi na washirikiane hata kutengeneza filamu ya pamoja.
Naamini wakiweka pembeni hizi Team, wakaacha kusikiliza maneno ya kinafiki yanayoundwa na baadhi ya wasanii wasiopenda urafiki wao, basi wataishi vizuri na watafanya kazi zao pamoja!