Malaysia imeanza awamu nyingine ya kuisaka ndege yake iliyopotea MH-370 kusini mwa bahari ya Hindi ikiwa ni takribani miezi saba tangu kutoweka kwa ndege hiyo. Meli iliyofungwa vifaa maalumu vinavyotumia teknolojia ya Sonar.Hata hivyo meli hiyo ikiwa na vifaa hivyo imewasili katika eneo la pembezoni kabisa mwa Bahari ya Hindi kilomita 18,000 magharibi mwa Australia.
Utafutaji wa ndege hiyo ulisitishwa kwa muda kwa kipindi cha miezi minne ili kutoa nafasi uchunguzi zaidi wa ramani kuhusiana na kupotea kwa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilipotea mwezi march mwaka huu wakati iliporuka kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.