Habari za ndani kutoka kambi ya Simba SC, zinasema Ivo Mapunda ataanzia benchi mtoto huyo wa kipa wa zamani wa Yanga SC, Manyika Peter akipewa dhamana ya kulinda lango la Wekundu wa Msimbazi.
Manyika mdogo atasaidiwa na mabeki, kulia William Lucian ‘Gallas’, Mohamed Hussein 'Tshabalala' kushoto na katikati Hassan Isihaka na Joseph Owino, wakati Jonas Mkude atakuwa kiungo mkabaji.
Ivo Mapunda ataanzia benchi leo, akimpisha Peter Manyika |
Viungo wachezeshaji watakuwa Said Ndemla na Amri Kiemba, wakati viungo wa pembeni watacheza Haroun Chanongo na Emmanuel Okwi huku mshambuliaji akiwa mmoja, Elias Maguri.
Katika mfumo huo, Kiemba atakuwa na jukumu la kusaidia katikati timu inapopoteza mpira na wakati huo huo kucheza kama mshambuliaji wa pili timu inaposukuma mashambulizi.
Kwa upande wa Yanga SC, langoni anaendelea Deo Munishi ‘Dida’, kulia Juma Abdul, kushoto Oscar Joshua, katikati Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati Mbuyu Twite atacheza kama kiungo wa ulinzi.
Viungo wachezeshaji watakuwa Hassa Dilunga na Haruna Niyonzima wakati viungo wa pembeni watakuwa Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho na Genilson Santana Santos ‘Jaja’ ndiye mshambuliaji.
Unaweza kuona timu zote zinatarajiwa kuwa na mifumo sawa katika mchezo huo- zikitumia viungo watatu katikati, mawinga kila upande na mshambuliaji mmoja.
Vikosi vinatarajiwa kuwa;
Simba SC; Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi, Said Ndemla, Elias Maguri, Amri Kiemba na Haroun Chanongo.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga, Genilson Santana Santos ‘Jaja’, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.
-BIN ZUBEIRY