Tuesday, November 25, 2014

BREEKING NEEEWS..!! WATU ZAIDI YA 5 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA HIACE KUTOKA KAHAMA-SHINYANGA KATIKA ENEO LA BUHANGIJA MJINI SHINYANGA

Hiace iliyopata ajali ikiwa eneo la tukio huku ikiwa imeharibika vibaya-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
Gari ikiondolewa eneo la tukio
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa na maafisa wa polisi mkoa wa Shinyanga eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
Watu watano wanadaiwa kupoteza maisha  leo majira ya saa tano asubuhi baada ya gari ndogo Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikitoka Kahama kwenda Shinyanga Mjini kupinduka katika eneo la Kona ya Buhangija mjini Shinyanga.

Walioshuhudia wanasema hiace hiyo ilikuwa katika mwendo kasi ikifukuzana na Hiace nyingine ndipo ikamshinda dereva wake baada ya kupiga Bamz ya Buhangija na kupinduka mara tatu.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema wameondoa miili mitano ya marehemu katika gari hiyo.
Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.


Tutakuletea taarifa kamili hivi punde kuhusu idadi kamiliya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo na idadi ya majeruhi.