Sunday, November 30, 2014

DIAMOND PLATNUMZ ANYAKUA TUZO TATU ZA CHANNEL O MUSIC VIDEO AWARDS 2014 ( CHOAMVA14 )


November 29, haitakumbwa kwenye maisha ya Diamond Platnumz na familia yake pekee, bali pia kwenye muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, baada ya hitmaker huyo wa ‘Number One’ kunyakua tuzo tatu kwenye tuzo za Channel O.

Diamond alikuwa ametajwa kwenye vipengele vinne. Vipengele hivyo ni pamoja na Most Gifted East Video, Most Gifted Afro Pop Video na Most Gifted Newcomer.
 
Kwenye tuzo hizo Diamond amefanikiwa kuwapiku wasanii nguli wa Afrika wakiwemo Iyanya, Davido, Flavour, Mafikizolo na Sauti Sol.
 
Ushindi huo umepokelewa kwa furaha kubwa na Watanzania wakiwemo wasanii wenzake.
 
“TANZANIA STAND UP! HE DID IT! @diamondplatnumz,” ameandika Davido.
 
“@diamondplatnumz wow congrats bro 3rd award already!! #cocobaby,” ameandika msanii wa Nigeria, Waje.
 
Naye Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa mpenzi wake ameandika:
 
“Tanzania kwanza. Hongera sana @diamondplatnumz ….. Una vitu vyako vingi vya sijui project hiki an kile lakini kwenye ukweli naongea na siku zote mimi nakubali wewe una 1. Jitihada 2. Vision/Muono wa mbali 3. Kipaji ….. From Tandale to the World. You are a true inspiration. Watoto wengi sasa hivi wataamini wanaweza kufanikiwa kwasababu ya njia ulioweza kuionyesha wewe kwenye kazi zako. Keep on shining bruh. Tanzania tuko nyuma yako wewe na nyuma ya wale wote wenye vipaji na jitihada. It’s time Tanzania tukatoa vipaji zaidi na zaidi tukaweka team za ushabiki ambazo hazijengi pembeni na kujenga umoja utakaotuwezesha ku-take over Afrika na dunia nzima. Tanzania tunaweza. Haya usiku mwema. ”
 
Hitmaker wa Doc Shebeleza, Casper Nyovest naye amenyakua tuzo tatu, Most Gifted South Video, Most Gifted Male Video Doc na tuzo kubwa ya usiku huo, Most Gifted Video of the Year.
 
Hii ni orodha nzima ya washindi:

Most Gifted Video of the Year
Doc Shebeleza – Casper Nyovest

Most Gifted Male Video
Doc Shebeleza – Casper Nyovest

Most Gifted Female Video
Eminado – Tiwa Savage

Most Gifted Afro Pop Video
Number One – Diamond Platnumz

Most Gifted South Video 
Doc Shebeleza – Casper Nyovest

Most Gifted East Video
Diamond

Most Gifted West Video
‘Turn Up’ – Olamide

Most Gifted duo/group/featuring
Pull Over – KCEE f/ Wizkid

Most Gifted Kwaito
Uhuru ft Oskido & Professor

Most Gifted RnB Video
‘Crazy But Amazing’ – Donald

Most Gifted Hip hop Video
Congratulate – AKA

Most Gifted Dance Video
Ngoku – Busiswa

Most Gifted Newcomer
Diamond Platnumz

Most Gifted Ragga Dancehall

Buffalo Souljah