Saturday, November 29, 2014

KABURI LA KUAMBIANA LAZIDI KUBOMOKA

INASIKITISHA! Tofauti na makaburi mengine ya wasanii mbalimbali wa filamu yaliyopo Kinondoni jijini Dar, la marehemu Adam Kuambiana limeendelea kubomoka na kuwa na mashimo huku likionekana kutelekezwa.
Kaburi la marehemu Adam Phillip Kuambiana.
Gazeti hili lilitembelea makaburini hapo na kushuhudia kaburi hilo likiwa na mashimo mengi pembeni tofauti na yale yaliyowahi kuripotiwa awali na magazeti Pendwa hivyo kutoleta picha nzuri kwa wasanii wenzake.
Akizungumza msanii mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema wasanii ambao walikuwa wakifanya kazi na marehemu hawafanyi vizuri kwani wana uwezo wa kujichangisha na kulijenga kaburi hilo kama alivyofanya Jeniffer Kyaka ‘Odama’ alivyotoa mchango mkubwa kulijengea kaburi la Recho.
Sehemu ya kaburi hilo ikiwa imeharibika.
“Kusema kweli wasanii waliofanya kazi kwa karibu na marehemu wajitahidi walijengee,” alisema msanii huyo.