Thursday, November 6, 2014

KAMA UNATAKA KUJUA UMEBAKIWA NA SIKU NGAPI ZA KUISHI DUNIANI.. HII HAPA NJIA RAHISI

Unahitaji kujua umebakiwa na
siku ngapi za kuishi duniani? Ipo
app ya simu itakayokupa jibu
hilo…
Ukuaji wa teknolojia unazalisha stori mpya kila
siku ila leo huenda ukashtuka; unajua simu
yako inaweza kukwambia siku yako ya kufa?
‘Macabre iPhone App’ ni application ambayo
unaweza kuiweka kwenye simu yako na
jukumu ambalo utakuwa nalo ni kuweka ratiba
zako zote za siku nzima, application hiyo
inapiga hesabu halafu inakupa majibu siku
zako ngapi zimesalia kuishi duniani.
Kali zaidi ni kwamba majibu utakayopewa ya
idadi ya miaka, miezi, wiki, siku na saa
itakuwa inaonekana kwenye screen lock, kwa
hiyo kila unapotoa lock ya kwenye screen
itakuwa inaonekana hapo juu.
Majukumu yako ya siku ndiyo yataakayoamua
siku ngapi utaishi.
Application hiyo inapatikana kwa simu za
Apple zinazotumia iOS na Windows 8.
Unadhani uko tayari kuitumia application hii?