Saturday, November 29, 2014

Kilichosemwa na Kamanda Kova na Waziri Lazaro Nyalandu kuhusu ajali ya Helikopta (Picha+Story)

helicopter-193569_640Taarifa ambayo imeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni kuhusu watu wanne kufariki kutokana na ajali ya Helikopta inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye namba 5HTWA kuanguka katika eneo la Kipunguni B, Ukonga Dar es salaam.
Akizungumza na kituo cha ITV Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa kamili juu ya tukio hilo muda mfupi ujao.
 Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Maliasili na Utalii  ameandika hivi; “Naelekea Dar kutokea Dodoma kwenda kwenye eneo la tukio la ajali ili kuwapa pole wafiwa. Nitazidi kuwafahamisha.”

Hizi ni baadhi ya picha kutoka eneo la tukio.IMG-20141129-WA0011

IMG-20141129-WA0016 (1)
IMG-20141129-WA0020
IMG-20141129-WA0022
IMG-20141129-WA0023