Monday, December 1, 2014

DIAMOND AFUNIKA CHANNEL O, SASA KUPELEKA TUZO ZAKE 3 DAR LIVE

Na John Joseph
STAA wa wimbo wa Nitampata Wapi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, juzi usiku alifanikiwa kuweka historia baada ya kutwaa tuzo tatu katika Tuzo za Video za Channel O (Channel O Music Video Awards 2014).
Diamond ambaye alikuwa ameongozana na Watanzania wengi kwenye usiku wa utoaji tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Nasrec Expo Centre Afrika jijini Johannesburg, Afrika Kusini, alikuwa karibu na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ pamoja na Zarina Hassan ‘Zari’, raia wa Uganda.
Hiyo ina maana kuwa, Diamond ametwaa tuzo tatu kati ya nne ambazo alikuwa akiwania, tuzo pekee aliyokosa ni ile ya Most Gifted Video of the Year (Video Bora ya Mwaka) ambayo ilitua kwa Carsper Nyovest kupitia wimbo wake wa Dos Shebeleza.
Katika usiku huo wa tuzo hizo ambazo pia ni maarufu kwa jina la CHOMVA 2014, Diamond alibeba ‘ndoo’ katika vipengele vya: Most Gifted East, Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer, zote zikitokana na wimbo wake wa Number One.Vipengele alivyobeba Diamond ni:
Most Gifted Newcomer (Msanii Bora Chipukizi)
Dream Team – TsekedeCassper Nyovest – Doc Shebeleza
Emmy Gee - Rands And Nairas
Diamond – Number One
Patoranking – Girlie O (Remix)
Most Gifted Afro Pop (Wimbo Bora wa Afro Pop)
Davido – Aye
Mafikizolo Ft May D – Happiness
Diamond – Number One
Flavour - Ada Ada
Iyanya – Jombolo
Zarina Hassan ‘Zari akiowa na tuzo alizoshinda Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Most Gifted East (Wimbo Bora wa Afrika Mashariki)
Sauti Sol – Nshike
Diamond – Number One
Navio – No Holding Back
Eddy Kenzo – Sitya Loss
Elani – Kookoo
Diamond Live jukwaani
Kutoka na ushindi huo, Diamond ambaye mara nyingi alisikika akiwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono katika kumpigia kura, anatarajiwa kuzionyesha tuzo hizo katika shoo kubwa ya Usiku wa Wafalme itakayofanyika Desemba 25, 2014 kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Shoo hiyo ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom na Coca Cola, itakuwa na mastaa wakubwa wawili ambao ni Diamond na Mzee Yusuf, hivyo Diamond anatarajiwa kutoa shukrani zake kwa Watanzania siku hiyo.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarina Hassan ‘Zari.
Wema amsifia kaka Diamond
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, muda mfupi baada ya Diamond kutwaa tuzo hizo, mpenzi wa zamani wa Diamond, Wema Sepetu, aliandika: “…Hongera tele ziende kwa kaka Platnumz, hakika ameifanya Tanzania ijivunie…”
Zari awa ubavu wa Diamond 
Zari ambaye alikuwa nchini hivi karibuni, ndiye aliyekuwa ubavuni mwa Diamond kila alipoenda kwenye shughuli hiyo kiasi kwamba kila mmoja alijua ndiye shemeji yetu mpya bila kipingamizi, japokuwa Diamond hajawahi kukiri hilo zaidi ya kusema wapo kwenye projekti.
Davido amsifia Diamond
Davido aliondoka mikono mitupu licha ya kuwa alikuwa kwenye vipengele vingi, alimsifia Diamond na Tanzania kwa jumla, jambo hilo lilisababisha Watanzania wengi wafurahi na kumpongeza Davido kwa wingi. Mastaa wengi pia wa Tanzania walimpongeza mtoto huyo wa Tandale kwa kuliwakilisha vizuri taifa.
Kumbukumbu
Watanzania wengine ambao waliwahi kushinda tuzo za Channel O katika miaka ya hivi karibuni ni Juma Nature (Mugambo - Wimbo Bora Afrika Mashariki 2007) na Witness (Zero - Wimbo Bora wa Afrika Mashariki 2008).