Monday, December 1, 2014

KAULI YA SHILOLE: BILA KIUNO NISINGEFIKA ULAYA!

MSANII wa muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kwamba shavu la shoo alilopata la Bara la Ulaya limetokana na kukata kwake kiuno hivyo mashabiki kuvutiwa naye. 
Msanii wa muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na AT, Uingereza. 
Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili akiwa barani humo anakoendelea kufanya shoo, Shilole alisema juhudi zake binafsi ndizo zilizompa shoo huko na hakutafutiwa na mtu yeyote pia anamshukuru Mungu kwani ameweza kuliteka soko la nje.
Kiuno changu na muziki ninaoimba ndiyo umenifanya nikapata shoo za Ulaya na juhudi zangu pia hapa nina shoo nne ambapo nitarudi Bongo Desemba baada ya kuzimaliza,” alisema Shilole.