KUNA mengi ya kushangaza duniani lakini hili la kijana Hamad Issa (32) kunaswa faragha na bibi kizee Adela Mkalau (80) linaongeza rekodi ya mambo yanayoshangaza, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu.
Tukio hilo la kustaajabisha limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, nyumbani kwa bibi huyo, Yombo –Buza, jijini Dar es Salaam ambapo wajukuu wa bibi huyo ndiyo waliomnasa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajukuu wa bibi huyo walifedheheshwa na kitendo hicho hivyo kuwawekea mtego na kuwanasa kisha kumfikisha Hamad katika Kituo cha Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za ubakaji.
BIBI: SIJABAKWA
Katika kutafuta uhakika wa madai ya wajukuu hao, polisi wa Chang’ombe waliagiza bibi yao aitwe ili athibitishe madai hayo wakati upelelezi mwingine ukiendelea.
Sosi wetu alisema kuwa bibi aliwaacha hoi polisi baada ya kufika kituoni hapo na kukataa maelezo ya wajukuu zake, huku akisisitiza hakubakwa bali walikubaliana na Hamad.
Baada ya bibi huyo kuondoa utata, polisi walikubali kumuachia Hamad kisha wajukuu wakafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhuru mwili iliyoandikishwa kituoni hapo kwa jalada namba CHA/RB/10629/2013.
BIBI NA PAPARAZI WETU
paparazi wetu alifunga safari hadi nyumbani kwa bibi huyo na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Sijabakwa na nimekasirishwa sana kwa kitendo cha kumpiga kijana wangu. Wawe na heshima kwa babu yao. Sisi tunapendana, kwa nini wanatuingilia?”
Alisema: “Siku hiyo Hamad wangu alikuja nyumbani kwangu tangu mapema. Nikaandaa chakula cha jioni, tukala pamoja kisha tukalala.
“Tukiwa usingizini, nikasikia mlango unagongwa. Kwenda kufungua, wajukuu zangu wakaingia na kuanza kumpiga Hamad na fimbo na magongo, wakisema eti amenibaka. Hamad atanibakaje? Kwani mimi ni mtoto mdogo?
“Isitoshe wanamfahamu vizuri sana Hamad. Nipo naye mwaka mmoja na nusu sasa, leo inakuwaje wanajifanya hawamjui? Siku hizi mambo yamebadilika. Mdogo anaweza kumpenda mkubwa na mkubwa akampenda mdogo. Hakuna kosa.”
MSIKIE DOGO
Mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa Hamad ambapo alimkuta akiwa hoi kitandani kwa majeraha ambapo alisema: “Ni kweli bibi ni mpenzi wangu... na wale wajukuu zake wananifahamu vizuri sana. Wamenipiga sana, eti nimembaka bibi yao. Siyo kweli. Sisi ni wapenzi.”
Alipoulizwa anajisikiaje kuwa kwenye uhusiano na kikongwe huyo, alijibu: “Hata mimi nashangaa sijui imekuwaje nikampenda. Nimejikuta nipo kwenye uhusiano naye na kwa kweli tunapendana sana.”
WAJUKUU WANASEMAJE?
Mmoja wa wajukuu wa bibi huyo, Margaret Cheba, akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo alisema bibi yao amewadhalilisha sana na wanaona aibu kupita mitaani kwa kitendo cha kutembea na Hamad.
“Hili jambo limetufedhehesha sana sisi wajukuu zake halafu hata kimila ni tatizo, hairuhusiwi kabisa. Mbaya zaidi, bibi yetu ni mgonjwa.
Anasumbuliwa na moyo... sio wa kufanya kitendo kama kile kabisa na sisi ndiyo tunamsaidia lakini inashangaza polisi wametubadilikia kabisa,” alisema Cheba.