Mdogo wake na Zari Hassan aka The Bosslady, aitwaye Karim ametumia Facebook kumkosoa dada yake kwa kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz ambaye anamzidi miaka 9.
Kwenye post hiyo, Karim aliandika: You are ashaming us, how can you date a boy my age. You moved from one man to another in less than 3 days.”
Akitumia akaunti yake binafsi ya Facebook yenye jina ‘Zarinah Tlale’, kujibu post hiyo ya mdogo wake huyo ambaye hapendezwi na kitendo cha dada yake kuwa na uhusiano na mtu mwenye umri kama wake, Zari alisema si Karim aliyeiandika.
“Diamond is just a friend of mine. It’s never been written that female and male can’t be friends, it’s just the backward people that use that kind of perspective to blow things out of proportion,” aliandika.
Katika hatua nyingine baada ya kumsindikiza Diamond kwenye tuzo za Channel O, Jumamosi iliyopita, Zari alimpa kampani pia kwenye utengenezaji wa video ya wimbo alioshirikishwa na kundi la Nigeria, Bracket.
Sh