Friday, December 26, 2014

MISS TANZANIA NAMBA 3 AFUNGUKA JINSI UMISS UNAVYOMPA STRESS


Miss Tanzania namba 3 (2014), Dorice Mollel.
MISS Tanzania namba 3 (2014), Dorice Mollel, amesema mashindano ya u-miss ni ‘stress’ tupu hivyo kama mrembo anataka kuingia ni lazima kujidhatiti na kukubali changamoto 
nyingi.Akizungumza na mwandishi wetu, Dorice alisema kuwa siku zote mrembo anapoingia kwenye shindano hilo madhumuni yake ni kushinda na si vinginevyo sasa inapotokea akaanguka maumivu yake yanatesa yanaweza kumkosesha amani kwa muda mrefu.
“Asikwambie mtu kabisa kwenye mashindano ya u-miss ni stress tupu jamani  kuanzia unaanza kujifunza hadi pale anapotangazwa mshindi halafu wewe ukakosa taji, inauma sana,” alisema  Dorice.