Mwandishi wetu
Staa wa filamu mwenye mvuto wa kipekee Shamsha Ford, amefunguka kuwa anatamani sana kuzaa mtoto mwingine lakini bado anaumiza kichwa ni nani atakayezaa naye mtoto huyo ili isije ikatokea kama mwanzoni kwa baba wa mtoto wake. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsha alisema hakuna kitu ambacho anakipenda kama watoto na pia kazi ya kulea anaifahamu vizuri sana hivyo alitamani mno kuongeza mtoto mwingine japo awe nao wawili.
Staa wa filamu mwenye mvuto wa kipekee Shamsha Ford.
“Yaani natamani mtoto sana lakini jamani nazaa na nani maana hapo ndipo pa muhimu kuangalia kwa kuwa mwanzo naona baba hakuwa sahihi japokuwa mtoto wangu nampenda sana,” alisema Shamsa.