Wachezaji wengi wa soka barani ulaya wamekuwa mstari wa mbele kuwatakia mashabiki wao heri ya sikukuu ya krismasi katika kipindi hiki ambacho kila mmoja amekuwa katika mzuka wa sikukuu hii .
Wachezaji hawa kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kama Facebook , Twitter na Instagram wamekuwa wakionyesha ubinadamu wao kwa kutuma ujumbe wa aina mbalimbali wa kuwataka mashabiki wao kuwa na furaha katika kipindi hiki .
Kwa beki raia wa Ujerumani anayecheza kwenye klabu ya Stoke City Robert Huth hali imekuwa tofauti baada ya mchezaji huyo kuonyesha hisia za kinyume kabisa na wachezaji wengine .
Mchezaji huyu aliustaajabisha ulimwengu kwa kitendo chake cha ku-tweet hisia zake kuhusiana na sikukuu hii ambayo inadhimishwa ulimwenguni kote.
Robert Huth kwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter aliandika kuwa anaichukia krismasi na hakutoa sababui za msingi za chuki aliyo nayo kwa sikukuu hii .
Hakuna aliyeweza kufahamu chanzo hasa cha utofauti huu toka kwa beki huyu Mjerumani ambaye amejijengea sifa kama beki mgumu asiyetetereshwa na washambuliaji awapo uwanjani .