Monday, January 26, 2015

ALI KIBA AKANA KUJIHUSISHA NA IMANI ZA KISHIRIKINA LEADERS

Tamasha lililofanyika Jumamosi iliyopita pande za Leaders limezua utata baada ya vituko vingi kutokea huku staa wa Bongo Fleva,Ali Kiba kuhusishwa na imani za kishirikina baada ya kushindwa kupita getini na kuruka ukuta.Mlinzi wa getini hapo amezungumza na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa Ali Kiba alifika getini lakini cha kushangaza hakupita mlangoni aliruka ukuta na kuingia ndani. ‘’Ali Kiba alifika hapa wenzake mimi nilikuwa hapa getini lakini nikashangaa ameruka ukuta’,alisema mlinzi huyo.
Hata hivyo haikuishia hapo habari zinasema kuwa Ali Kiba alishindwa kumpa mkono msanii mwenzake Mwana Fa huku baunsa wake akimzuia msanii huyo kumsalimia Ali Kiba.
Katika tamasha hilo mashabiki wa mastaa wawili Ali Kiba na Diamond Platinumz walifanya vurugu kwa kurusha chupa za maji baada ya wasanii hao walivyokuwa wakipanda jukwaani kupafomu