Kaci Fennell aliwataja Bob Marley na Usain Bolt kuwa watu waliotoa mchango mkubwa kwa dunia kutoka nchini mwake.
MISS Colombia, Paulina Vega atwaa taji la Miss Universe 2015 katika fainali zilizofanyika jana huko Miami nchini Marekani huku umati ukizomea kuonyesha kutoridhika na matokeo hayo.
Umati uliohudhuria fainali hizo ulitarajia Miss Jamaica Kaci Fennell aliyeshika nafasi ya nne kutwaa taji hilo lakini ulionyesha kushangazwa na maamuzi ya majaji kumtangaza Miss Colombia Paulina Vega mwenye miaka 22.
Zomea zomea zilisikika mara baada ya mshindi huyo kutangazwa huku kukiwa na minong'ono ya hujuma katika mashindani ya mwaka huu.