Monday, January 26, 2015

MAJAMBAZI YAULIWA WAKIJARIBU KUPORA FEDHA KARIAKOO

Majambazi yameuliwa na polisi jana kwenye
Makutano ya Mkunguni/Livingston street,
Walipojaribu kupora fedha kwenye Bureau De
change. ...........lakini Polisi waliwahi!
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo Kanda Maalum ya
Dar es salaam, imesema kuwa katika tukio hilo
majambazi wawili waliuawa kwa risasi wakati
wakijaribu kuwadhuru askari.
Tukio hilo lilitokea eneo la Kariakoo mtaa wa
Mkunguni na Livingstone saa 3.00hrs usiku.
Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na
mlalamikaji alikuwa anatumia taa za kawaida.
Mara baada ya kuanza tukio hilo la uporaji
wasamaria wema walijulisha Jeshi la Polisi ndipo
kikosi maalum cha kupambana na majambazi (ant
robbery squared) kilipofika kwa haraka katika eneo
la tukio tayari kwa mapambano.
Taarifa hiyo inasema kuwa Majambazi hao
walistuka na kuanza kuwarushia risasi askari
waliokuwa katika gari la Polisi na ndipo sasa
kukawa na mapambano ya moja kwa moja kati ya
pande hizo mbili kwa kutumia silaha na kurushiana
risasi. Hatimaye majambazi wawili waliuawa
mmoja anayejulikana kwa jina la ALLAN S/O
OCHENG @ ONYANGO, Miaka 24, raia wa Kenya
aliyepatikana na Pass ya kusafiria yenye nambari
A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini
Kenya.
Jambazi mwingine aliyeuawa ametambuliwa kwa
jina la YUSSUPH S/O HAMIS @ TWALIB, Miaka 46,
Mshiraz, Mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Majambazi wengine waliotoroka baada ya tukio hilo
wanaendelea kutafutwa na tunaomba raia wema
waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili
wapatikane.
Pamoja na kuuawa kwa majambazi hawa na
kukamatwa kwa silaha, pia zimekamatwa pikipiki
mbili moja ni SUNLG yenye namba za usajili T249
CMC, rangi nyekundu. Nyingine ni aina ya BOXER
yenye namba za usajili MC350 AM rangi nyeusi
ambazo zote zilitumiwa na majambazi hao katika
tukio.
Aidha, Jambazi ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO
aliyeuawa amekutwa na simu ya mkononi aina ya
TECNO.
MAJAMBAZI WENGINE TISA SUGU WAKAMATWA
JIJINI DAR ES SALAAM
Katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es
Salaam dhidi ya ujambazi wa kutumia silaha Jeshi
la Polisi limekamata majambazi tisa
wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ya
unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa ya
kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Oparesheni kali bado inaendelea jijini Dar es
Salaam ili kuhakikisha kwamba majambazi wote
wanaotumia silaha pamoja na makosa mengine
ambayo ni kero katika jamii yanashughulikiwa
kikamilifu. Pamoja na mafanikio hayo
tunawashukuru raia wema kutokana na juhudi zao
za kutoa taarifa mapema zenye kuwa na mafanikio
ya kulifanya jiji la Dar es Salaam liendelee
kuwashwari.