Wednesday, January 21, 2015

ANUNUA ‘bulletproof’ NA KUMJARIBISHIA RAFIKI YAKE, MATOKEO YAKE NI?? SOMA HAPA KILICHOMKUTA

target_shooting_by_fumikazu-d6pw3vw
Kila mtu anapenda kujiweka mazingira ya usalama, hakuna asiyependa ulinzi hata kidogo! Huyu bwana aliamua kujiwekea ulinzi wa ziada, akaenda duka la kijeshi Marekani ili akanunue bulletproof ili kujiongezea usalama na matukio yanayohusisha risasi.
graphene-may-make-better-bulletproof-vests (1)
Catley alinunua vest hiyo ya bulletproof, akaomba mtu wa kwanza aijaribu kama inafanya kazi poa, mtu huyo akakaaa, jamaa akaivaa jioni yake akaingia nayo Club wakajienjoy na rafiki zake, baada ya kulewa akawa anawaomba washkaji zake kadhaa ili aijaribu vest hiyo kama inafanya kazi, wapo waliokataa lakini rafiki yake ambaye ni Philip Harper alikubali kujaribiwa.
Hii ni moja ya tukio la majaribio ya bulletproof.
Hii ni moja ya tukio la majaribio ya bulletproof.
Bulletproof hiyo haikuzuia chochote, Cartley alimpiga rafiki yake huyo na kumjeruhi vibaya, akakimbizwa hospitali lakini alifariki na mahakama ikamhukumu kifungo cha miaka saba jela kwa kosa hilo.

Hivi mfano inakuwa ndio wewe unaweza kukubali kujaribiwa kwenye hii kweli? Unaweza kushare chochote kwa kucomment mtu wangu