Wednesday, January 21, 2015

MZEE CHILLO AMUONGOZA MGHANA KUMUANGUKIA MONA

MUIGIZAJI mkongwe,Ahmed Ulotu maarufu kama Mzee Chillo, hivi karibuni alimuongoza mtayarishaji wa filamu kutoka Ghana, Prince Richard kwenda kumpigia magoti mpenzi wake wa zamani, Yvonn Cherly ‘Monalisa’ baada ya kumkosea, lakini akajikuta akigonga mwamba kutokana na binti huyo kukataa.
 
Muigizaji mkongwe, Ahmed Ulotu maarufu kama Mzee Chillo.
“Mona alikuwa Tabata Segerea shooting akiwa na wasanii wenzake, Mzee Chillo alimfuata muda wa saa mbili usiku akiwa na ‘Director’ huyo bila Mona kujua, yeye aliambiwa kuna bonge la dili anapelekewa, walipomfikia, wakamwambia wasogee pembeni waongee ndipo Richard alipotoka kwenye gari na kumfuata ili amkumbatie, akakataliwa,” kilisema chanzo cha habari hii.
 
Msanii wa filamu Bongo, Yvonn Cherly ‘Monalisa’.
Inadaiwa kuwa Richard alimbembeleza sana Mona huku akitaka kumpigia magoti lakini aliendelea kutiliwa ngumu na mwisho alimwambia kuwa yeye hahitaji kumsamehe.
Monalisa, mke wa zamani wa mtayarishaji mwingine maarufu, marehemu George Otieno ‘Tyson’, alikiri kumuona Richard lakini akakataa kuongelea lolote kuhusu ishu hiyo.