Emmanuel Nelson akiwa wodini Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Nelson ambaye alishindwa kuongea akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alifikishwa na polisi wa kituo kidogo cha Pangani, Ilala, jijini Dar es Salaam, Januari 15, mwaka huu baada ya kumwokota barabarani, anasemekana alivunjwa taya hilo kwa kupigwa na watu wasiojulikana.
Mtu huyo ambaye amelazwa katika wodi ya Sewa Haji namba 23, amesema ameshindwa kupata Sh. 60,000/= kwa ajili ya gharama za matibabu na kulazwa ambapo amesema ametelekezwa na ndugu zake wanaoishi Tabata-Relini, jijini Dar es Salaam.
Nelson anahitaji kufungwa waya na matibabu mengine ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
Kwa yeyote aliyeguswa na tukio la mgonjwa anaweza kumchangia kupitia namba ya simu 0655 207 156, pia anaomba ndugu, jamaa na marafiki wajitokeze kumwona na kumsaidia.