Friday, January 2, 2015

APEWA MATUSI BAADA YA KUMBEBA MTOTO WAKE KWENYE POCHI NA KUIWEKA PICHA MTANDAONI!

mtoto bag 
Nchi za Mataifa ya Ulaya wamekua wakithamini sana wanyama kama mbwa na kuwafanya sehemu ya maisha yao ya kila siku.
 Mara nyingi wanapokwenda kwenye matembezi  hutumia pochi ama aina mbalimbali za bag kubeba mbwa kama sehemu ya utamaduni wao.
 Lakini hili tukio la mama huyu kutoka China mwenye miaka 26 Xue Hsueh limewashangaza watu wengi na kuona kama ni unyanyasaji na ukatili kwa mtoto baada ya kuamua kumbeba mwanaye wa miezi tisa katika pochi yake huku akidhani ni wazo zuri.
 dogg 
Kumbeba peke yake haikutosha kwani mwanamke huyo aliamua kupiga picha huku mwanaye huyo akiwa kwenye pochi na kuisambaza kwenye mitandao na alikutana na majibu yaliyomnyima raha kabisa baada ya watu kuchukizwa na kitendo hicho.
 Pamoja na kujitetea kwa maamuzi yake alisema alimbeba kwenye pochi kwa muda mfupi na pia alikua akiwatania marafiki zake kuwa ingekuwaje kwa mwanaume mwenye jukumu la kulea mtoto akiachiwa jukumu hilo.