ZIKIWA zimepita siku chache tangu mwaka wa 2015 uanze, mwanadada mwenye umbo matata Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ amekiri kuuanza vizuri baada ya kupima ngoma.Akipiga stori na gazeti hili, Anti Lulu alisema anafurahi kwa kuwa ameuanza mwaka vizuri baada ya kwenda kupima Ukimwi akiongozana na mama yake na kujikuta yupo salama.
Mwanadada mwenye umbo matata Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ akipozi.
“Yaani nina furaha ya ajabu baada ya kukutwa niko mzima kwani nilikuwa na wasiwasi sana kutokana na njia nilizopitia kutokuwa salama, mama yangu ndiye aliyenishauri na kunisindikiza hospitali, nawasihi wasanii wenzangu nao wakapime ili wagundue afya zao na waweze kuishi bila wasiwasi,” alisema Anti Lulu.