NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ anadaiwa kumpiga paparazi (wa blogu moja maarufu) kwa madai ya kuwa aliwahi kumpiga picha akiwa mahakamani kipindi alipokamatwa na dawa za kulevya.
‘Chid Benz’ akiwa mahakamani kipindi alipokamatwa na dawa za kulevya.
Tukio hilo lilitokea Jumapili katika Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar, ambapo Kundi la Yamoto Band walikuwa wakizindua wimbo wao mpya wa Itanipwelepweta, Chid Benz naye alikuwepo maeneo hayo na baada ya shoo alifuatwa na baadhi ya mapaparazi kwa ajili ya mahojiano.
Akizungumza na gazeti hili paparazi huyo alisema kitendo cha mapaparazi kukusanyika mbele yake Chid alionekana kukumbuka kitu na kuanza kumpiga vibao.
“Alipomaliza kunipiga vibao alitoka nje na kuwaita watu waje wanipige, wameniumiza sana mbali na kujitetea waliendelea kunipiga mpaka pale alipokuja Babu Tale kuamua ndipo ugomvi ukahamia kwake na Chid akaanza kuvua fulana, cheni na kumpa mtu amshikie na kutaka kupigana na Babu Tale tena,” alisema.
Gazeti hili lilimtafuta Babu Tale na baada ya kusikia madai hayo alikana na kusema hataki kuhusishwa na ugomvi huo na mpaka gazeti linaenda mtamboni Chid alikuwa hapatikani hewani.