DOKTA mmoja wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar (jina lipo) ameibuka na kumtaka Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ aliyewahi kubeba jukumu la kuitengeneza afya ya Mbongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ asimamie tena jukumu hilo ili kuokoa maisha ya msanii huyo.
Dokta huyo aliyasema hayo juzi katika mahojiano na Amani kufuatia madai kwamba, Ray C hana mahudhurio mazuri kwenye kliniki ya kuchukua dawa za kuponya mtu aliyeathirika na matumizi ya madawa ya kulevya au maarufu kwa jina la ‘unga’.
“Jamani, naamini mnajua kuwa Ray C anatibiwa katika kliniki ya waathirika wa madawa ya kulevya hospitalini kwetu lakini mimi sifurahii mwenendo wake kwa ujumla.“Ray C haendi sawasawa katika tiba. Ni hatari kwake, tena hatari sana.“Dada yetu huyu aliacha kabisa kutumia haya madawa kipindi fulani lakini sasa mwenendo wake kwenye kliniki si mzuri.
“Hizi habari tumezipata kutoka kwa wenzake anaotumia nao dozi. Unajua wale hawana siri. Ray C anatumia dawa za Methadone kama kawaida. Lakini nahofia kama mwenendo wake utakuwa kama zamani, Methadone ni hatari kwani haichanganywi na sumu nyingine mwilini,” alisema dokta huyo.
Akaongeza: “Mtu akiacha matumizi ya madawa ya kulevya na kuanza kutumia Methadone ambazo zinadumu kwa muda wa saa 24 hadi 26 mwilini kwa kutumia dozi moja kwa siku, akitumia kitu chenye sumu inakuwa ni hatari katika maisha.
Baadhi ya madawa ya kulevya yanayogharimu nguvu kazi ya Taifa.
AMWONYA RAY C
Dokta huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, anamwonya Ray C, kutokuwa mhudhuriaji mzuri kliniki asije akajikuta anabobea katika matumizi ya unga kwani kwa kufanya hivyo atakaribisha hatari ya maisha yake.
Dokta huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, anamwonya Ray C, kutokuwa mhudhuriaji mzuri kliniki asije akajikuta anabobea katika matumizi ya unga kwani kwa kufanya hivyo atakaribisha hatari ya maisha yake.
“Ray C asije akabobea tena kwenye unga. Unga na Methadone ni vitu viwili tofauti kabisa. Ukitumia Methadone halafu ukatumia unga, dozi ikizidi kifo ni nje nje,” alisema dokta huyo.Aliongeza kusisitiza kwamba, utaratibu alioutumia JK kumsaidia awali Ray C anamwomba chondechonde kurudia tena na safari hii ampe usimamizi wa hali ya juu.
Kufuatia taarifa hizo, Amani juzi hiyohiyo lilimtafuta Ray C kwa njia ya simu ambapo alipoulizwa kuhusu mahudhurio yake hafifu kliniki, alikuja juu akisema si kweli.Amani: ”Au utakuwa umerudia mambo yale Ray C? Inawezekana kweli?”Ray C: “Si kweli nimesema, we andika uone nitakachowafanyia, nitawafikisha mahakamani na kuwamaliza.”