Wednesday, January 7, 2015

CHANZO CHA UGOMVI WA MESSI NA KOCHA WAKE HIKI HAPA.

messio
Habari za kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya nyota wa BarcelonaLionel Messi na kocha wake Luis Enrique mpaka sasa sio mpya masikioni mwa mashabiki wa soka barani ulaya baada ya matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea ndani ya klabu hiyo ya Nou Camp.
Tetesi zaidi zinadai kuwa kocha Luis Enrique amepewa mechi mbili kuokoa kazi yake jambo ambalo Barcelona imekanusha laki ni hakuna asiyefahamu kuwa Messi na kocha wake hawaelewani.
Chanzo cha ugomvi baina ya wawili hao kimefahamika baada ya ripoti kadhaa toka kwa watu walioko karibu na klabu hiyo kufichua kuwa ugomvi huu ni mkubwa kuliko inavyodhaniwa na umefikia hatua mbaya.
Messi na Luis Enrique walikuwa karibu kupigana mazoezini siku ya ijumaa ya wiki iliyopita.
Messi na Luis Enrique 
Ripoti tofauti zinasema kuwa Messi na kocha wake waligombana siku ya ijumaa wiki iliyopita na ugomvi ulikuwa mkubwa kiasi cha wawili hao kukunjana na kutaka kupigana kabla ya kuachanishwa na wachezaji wa Barcelona.
Messi ambaye alichelewa kujiunga na kambi ya Barcelona baada ya kutoka kwenye mapumziko nyumbani kwao Argentina aliingia mazoezini siku hiyo ya ijumaa na kuungana na wenzie ambao walikuwa wakifanya mazoezi ya kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe huku Enrique akiwa refa.
Kiungo Mbrazil Neymar ndiye aliyewatenganisha wakati wakiwa wamekunjana.
Katika mazoezi hayo Messi alichezewa rafu ambayo alitaka kupewa adhabu ndogo lakiniEnrique hakupuliza filimbi jambo ambalo lilimkera Messi na kumfanya aanze kumshutumuEnrique.
Baada ya mazoezi hayo kumalizika Messi alimfuata Enrique na kuanza kutupiana nae maneno mpaka kufikia kukunjana kabla Neymar hajaingilia ugomvi huo na kuwatenganisha kabla hawajapigana.
Kufuatia ugomvi huu Enrique alimuacha Messi benchi kwenye mchezo uliofuata dhidi yaSociedad na nyota huyo alijibu mapigo kwa kutohudhuria mazoezi ya jumatatu.