Dunia haishi maajabu na maajabu yamekuwa yakitokea siku hadi siku na yanatokea karibu kila mahali .
Mwanamke mmoja huko nchini Marekani aitwaye Barbarella Buchner ametoa kali ya mwaka 2015 baada ya kufunga ndoa na paka wake wawili .
Mwanamke huyo alipokuwa anatoa ufafanuzi juu ya tukio hilo amesema kuwa hakuwahi kuwa na wazo la kuolewa na mpenzi yoyote yule wa kiume kati ya wapenzi alio nao na hajawahi kuwa na wazo kwamba atakuja kuwa mke wa mtu au kiumbe yoyote yule .
Barbarella mwenye umri wa miaka 48 ambaye kazi yake ni ubunifu wa tovuti kwenye mtandao wa internet ameongeza kuwa ana furaha kubwa baada ya kuolewa na paka wake wawili ambao ameolewa nao .
Mwanamke huyo alinukuliwa akisema kuwa ‘kuna baadhi ya wanawake wamepangiwa kufanya usafi kwa ajili ya waume zao na wameridhia kufanya hivyo , kwangu ni tofauti’ alisema Barbarella .
Ameongeza kuwa haoni shida kuwatumikia paka wake ambao wana majina ya Lugosi na Spider na siku zote atahakikisha wanaishi kwa furaha kama ndoa inavyohitaji.
Mwanamke huyu hakuweza kufananua kama moja ya misingi muhimu ya ndoa ‘unyumba’ itahusika kwenye ndoa yake hiyo na paka wake wawili.