Wednesday, January 7, 2015

KIZAZI KIPYA CHA MAGARI KITAKUWA HIVI.

Mercedes-Benz at the Auto China 2012 in Beijing

Kampuni ya kutengeneza magari ya Ujerumani ya Daimler imejipanga kutengeneza gari ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe huku ikiwa na uwezo wa kuchukua abiria wanne .
Gari hii ambayo imeundwa kwa muundo wa kisasa itakuwa ya kipekee huku ikiwa na usukani kama magari mengine tofauti na lile gari la google ambalo halina usukani huku siti ya dereva na siti ya abiria ikiwa na uwezo wa kuzunguka na kufanya watu waliokaa kutazamana kama wako kwenye meza moja .
Sehemu ya ndani ya gari hii ambayo ina nafasi ya kukaa watu wakiwa wanatazamana.
Sehemu ya ndani ya gari hii ambayo ina nafasi ya kukaa watu wakiwa wanatazamana.
Gari hii aina ya Mercedez Benz Luxury Sedan F 015 bado haijapangiwa tarehe ya kutengenezwa na kuzinduliwa lakini kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Daimler ambaye alikuwa anaelezea gari hilo huko Las Vegas kizazi kijacho cha magari kitakuwa na magari ambayo yana uwezo wa kumpa kila mtu fursa ya kustarehe wawapo ndani ya gari .
APTOPIX Gadget Show Mercedes Benz

Mercedes-F125-Hydrogen-Concept