Manchester United inatarajia kumtangaza kipa Mhispania Victor Valdez kama usajili wake wa kwanza wa mwezi huu januari wakati dirisha dogo la usajili likiwa wazi baada ya ya kipa huyo kufanya mazoezi na United kwa zaidi ya miezi miwili .
Valdez alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na United ili ajiweke sawa baada ya kupona jeraha la goti ambalo limemsumbua kwa muda mrefu tangu alipokuwa na klabu ya Barcelona katikati ya msimu uliopita .
Valdez alikuwa kwenye mipango ya kukamilisha uhamisho kuelekea klabu ya As Monaco kabla klabu hiyo haijafanya maamuzi mengine na kuachana naye hali iliyomfanya akose klabu baada ya kuachana na Barcelona msimu uliopita.
Usajili wa Valdez utaifanya United kuwa na makipa wawili raia wa Hispania baada ya kipa wake namba moja ambaye ni David De Gea ambaye hadi sasa amekuwa kwenye kiwango cha juu ndani ya klabu hiyo .
Zaidi ya De Gea idadi ya wachezaji wa Kihispania kwenye kikosi cha kwanza cha United inatarajia kufika wachezaji wanne baada ya Ander Herrera na Juan Mata ambao wamekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha United msimu huu .
Usajili wa Valdez utafuatiwa na kuondoka kwa kipa namba mbili wa United Anders Lindergaard ambaye anatarjiwa kuondoka januari hii kutafuta timu ya itakayompa nafasi ya kuwemo kwneye kikosi cha kwanza huku pia ikiwa ni tahadhari ya kujiandaa na kuondoka kwa David De Gea ambaye tetesi zimemhusisha na kujiunga na Real Madrid