WAKATI staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, akitafutwa kufanya kolabo na wasanii mbalimbali, nyota wa muziki huo kutoka Moro Town, Dayana Nyange, ‘Dayna’ ameibuka na kusema hana mpango wa kufanya kazi na staa huyo hata kama anafanya vizuri kimataifa.
Akifunguka na Risasi Vibes, Dayna alisema kuwa hajaweka wazo la kumpa kolabo staa huyo kwani hajui kama kuna kazi ambayo anaweza kufanya vizuri ikiwa pindi atakapo mshirikisha, ingawa wapo ambao wanahitaji kufanya naye kazi.
“Kwa kweli sijapaga kufanya kazi na msanii huyo na kwangu sitazami eti anafanya vizuri nje na mimi nimpe kazi yangu hapana, nataka msanii ambaye anaweza kusimama kwenye ngoma yangu, bila hivyo bora nifanye mwenyewe,” alisema Dayna.