Wednesday, January 21, 2015

DIDA, EZDEN WAMEBAKI MARAFIKI TUU

WATANGAZAJI ambao walikuwa wanandoa kabla ya kuachana, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne wamemaliza tofauti zao na sasa wamekuwa marafiki sana kiasi cha kuzua minong’ono kwamba wamerudiana.
Watangazaji, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne wakati wakiwa wanandoa.
Baada ya minong’ono hiyo kuzidi, Risasi Vibes ilimtafuta Dida ili kueleza ukweli ambapo alisema ni kweli amemaliza bifu na Ezden na sasa ni marafiki lakini suala la kurudiana siyo kweli na halipo kabisa kwani tayari yeye ana mtu wake na Ezden pia ana mtu wake.
“Tumemaliza vinyongo tulivyokuwa navyo na sasa tuko kama watu wa kawaida lakini hakuna mapenzi tena na hatuwezi kurudiana. Pia kila mtu ana uhusiano mwingine, sisi ni marafiki tu watu waelewe hivyo,” alisema Dida.