Wednesday, January 21, 2015

SNURA ADAIWA KUMFICHA MWANAYE

MSANII nyota wa miondoko ya Mduara, Snura Mushi aliyekuwa kimya kwa muda mrefu kufuatia kuwa na ujauzito, amerejea jijini Dar akitokea Mbeya alikojifungua mtoto wa kiume, lakini kukiwa na madai kwamba anamficha mwanaye asionekane kwa watu.
Msanii nyota wa miondoko ya Mduara, Snura Mushi.
“Namshangaa sana huyu mwenzetu sijui anachomfichia huyo mtoto ni kitu gani, angeficha ujauzito watu tungeelewa labda sababu za uswahili, lakini mtu umeshajifungua unaogopa nini?” kilihoji chanzo chetu kilichodai kuwa Snura amejifungua mtoto wa kiume.
Mkali huyo wa kibao cha Majanga alitafutwa kwa simu yake ya mkononi, alitoa ushirikiano vizuri lakini alipoulizwa kuhusiana na madai hayo, aliruka kimanga, akidai kuwa yeye siyo Snura na kukata simu.