Huku habari kuhusu uhusiano mbaya wa Lionel Messi na klabu yake ukiendelea kutengeneza headlines kwenye vyombo vya habari barani Ulaya tetesi za kuondoka kwake zimezidi kushika kasi huku kila siku ikiibuka story mpya.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtaalamu wa biashara kwenye mchezo wa soka ni klabu mbili pekee ambazo kwa sasa zina uwezo wa kumsajili nyota huyu raia wa Argentina kinyume na ilivyoripotiwa kuwa klabu kadhaa ziko kwenye harakati za kumsajili.
Klabu hizi zimetajwa kuwa Manchester United na Real Madridkutokana na kuwa na msuli wa kifedha pamoja na sababu nyingine ambazo zinaleta ugumu kwa zile klabu ambazo zinaweza kuwa na fedha lakini zikashindwa kufanya usajili kutokana na kubanwa kwenye sehemu tofauti.
Katika hali ya kawaida klabu kama Manchester City, PSG , Chelsea naBayern Munich zinaweza kumsajili mchezaji yoyote kwa bei yoyote, lakini hali kwa sasa ni tofauti kwani kanuni za kusimamia matumizi ya fedha kwa vilabu ‘Financial Fair Play’ zinafanya matumizi kwa vilabu yafanywe kwa kuzingatia vitu vingi.
Hapa ndio mahali ambako United na Real zinapata faida endapo zitakuwa na dhamira ya kumsajili Messi.
Ili kumnunua Messi klabu inayomtaka itapaswa kulipa ada ya uhamisho ambayo ni paundi milioni 196 na mshahara wake utalazimika kuwa mkubwa kutokana na hadhi ya mchezaji mwenyewe na kwa mantiki hiyo ni United na Madrid pekee ambazo zinatengeneza aina ya fedha ambayo inaweza kutosha kumnunua Messi pasipo kukiuka sheria zaFinancial Fair Play.
Klabu ambazo zinatangaza hasara ya zaidi ya paundi milioni 23.5 kwa muda wa miaka mitatu zinaadhibiwa na sheria za FFP na tayari Man Cityna PSG zimekumbana na rungu hilo jambo ambalo linawaondoa kwenye mbio za kumsajili Messi endapo nyota huyo atawekwa sokoni.
Pamoja na ukweli huu bado haitakuwa rahisi kwa Barcelona kukubali kumuona Messi akiondoka hasa ukizingatia kuwa klabu hiyo ina adhabu ya kutofanya usajili kwa muda wa mwaka mzima hali inayowafanya wasiwe kwenye nafasi ya kumuuza mchezaji yoyote muhimu kwani kufanya hivyo itakuwa sawa na kujidhoofisha huku wakiwa hawana nafasi ya kujiimarisha.