Tumeona baadhi ya wasanii walioamua kuachana na ukapera na kuamua kuoa kama, yupo Noorah, Amini , Shetta, Steve RNB, muigizaji wa filamu Pasta Myamba, sasa time hii nakusogezea hii stori ya msanii kutokea Tip Top Connection, Khalid Ramadhani aka Tunda Man ambaye hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa.
Akizungumza na millardayo.com alisema;’Nimegundua ukiwa mwanamuziki kuna vishawishi vingi sana ninavyokutana navyo katika show, nakutana nazo Studio au barabarani unapotembea kwa hiyo nimegundua kwamba sisi watoto wa kiislamu kuna umri ukifika miaka 25 na kuendelea unatakiwa tu ukae na wifi mpange hiki na hiki na hiki.. na mimi hicho nimekigundua kwani nimesoma sana vitabu vya dini ya kiislamu kwasababu najua Mungu yupo na sisi tunasurvive kwasababu ya Mwenyezi Mungu na vitabu vya dini vinasema ukioa ni nusu ya uislamu na ukiwa ujaoa bado haujafika hata nusu ya Uislamu
Kwa hiyo nimeona kwanini nisije nikafa bure hata nusu ya Uislamu sijafika nitaenda kumjibu nini mwenyezi Mungu kaburini, kwa hiyo nimeona atleast nifike hata nusu ya uislamu… Natarajia kuoa soon nafikia mwezi wa pili sitaki kuleta sherehe nyingi sitaki kuleta mbwembwe… Ikishafika tarehe 14 na kuendelea mfahamu kuwa nimeshaoa na vikao vimeshaanza kufanyika na Big boss Chief Kiumbe ameniambia atagharamia kila kitu kuanzia mahari mpaka harusi“–Tunda Man.