Monday, January 19, 2015

JEZI MPYA ZA MANCHESTER UNITED ZA MSIMU UJAO ZAANZA KUWA GUMZO

An apparent leaked Manchester United shirt for next season is doing the rounds on Twitter 
Huku msimu ukiwa katikati, tayari suala la jezi mpya za Manchster United kwaajili ya msimu ujao zimeanza kuwa gumzo.
Adidas ndio watakaotengeneza jezi mpya za timu hiyo kufuatia mkataba wake mnono wa utakaoiingizia United pauni milioni 700 kwa kutumia vifaa vya michezo vya Adidas.
Dili hilo linahitimisha miaka 13 ya kampuni nyingine ya kutengeza vifaa vya michezo – Nike.
Huku Adidas wakiwa katika maandalizi ya kutengeneza ‘uzi’ mpya wa United, tayari muundo wa jezi mpya umesambaa kupitia mtandao wa Twitter (Tazama picha juu).
Hata hivyo Daily Mail limebaini kuwa jezi hiyo siyo halisi na kwamba sura ya jezi mpya ya Manchester United bado haijatolewa