Saturday, January 10, 2015

LULU APELEKEWA BARUA YA UCHUMBA

STAA ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amepelekewa barua ya uchumba kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Dar na kumfanya mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila abaki ameshangaa.Tukio hilo lilitendeka Januari 8, mwaka huu, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako ndiko yaliko makazi ya Lulu na mama yake huyo.
Mshenga anayefahamika kwa jina moja la Isaya akipeleka posa kwa akina Lulu Elizabeth Michael.
MSHENGA NI MPAMBE
Kwa mujibu wa watonyaji wetu ambao waliwataarifu mapaparazi wetu wa Kitengo cha Kufichua Maovu (OFM) kuhusu barua hiyo na kutia timu nyumbani hapo, mtu aliyepewa kuifikisha kwenye familia hiyo ni mpambe mkubwa wa mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Isaya, mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam ambaye sasa amekuwa mshenga pia.
Staa ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
MSHENGA GETINI KWA AKINA LULU
Ilikuwa saa tano asubuhi, mshenga huyo akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Corolla (namba hazikupatikana mara moja), alishuka nje ya geti kuu la nyumbani kwa akina Lulu ambapo anaishi na mama yake.
Mshenga huyo alibisha hodi kwa muda wa kama dakika tano ambapo mfanyakazi wa ndani (hausigeli) alifika getini na kufungua mlango.
Mshenga akigonga hodi getini kwa akina Lulu.
KILICHOZUNGUMZWA GETINI
Haikujulikana mara moja, wawili hao walikuwa wakizungumza nini getini lakini mapaparazi wetu waliweza kushuhudia mshenga huyo akinyoosha mkono na kumpa bahasha msichana huyo kisha geti likafungwa, mshenga huyo akasimama pembeni, huenda kusubiri majibu.
MSICHANA AREJEA
Baada ya dakika kama kumi, msichana huyo alirudi getini, akafungua nusu ya mlango kama awali na kuanza kuzungumza na mshenga huyo.
MSHENGA AONDOKA
Baada ya mshenga huyo kuondoka hatua kama ishirini mbele mapaparazi wetu walimwibukia na kumuuliza shida iliyompeleka kwenye nyumba ya akina Lulu.“Kwani vipi?” aliuliza mshenga huyo kabla ya kusema.
Mshenga akiondoka mara baada ya kumaliza majukumu mazito.
Risasi: “Sisi tulipata habari kwamba wewe umepeleka barua ya posa pale, ni kweli?”
“Kweli nimetoka nyumbani kwao na Lulu, nilipeleka barua ya uchumba ya bosi wangu.
“Nimefurahi nilipofika pale nikagonga geti, akatoka msichana mmoja, nilimuuliza kama mama Lulu yupo akasema yupo, nikampa barua akapeleka maana hakutaka mimi niingie,” alisema mshenga huyo.
MAJIBU YALIKUAJE?
“Baada ya muda yule msichana alirudi, akanipa barua akisema eti si ya Elizabeth wala Lulu. Sasa ni ya nani wakati jina la juu ya bahasha ni Elizabeth Michael.”“Naamini kabla mama Lulu hajaisoma aliangalia juu ya bahasha na kuliona jina la Elizabeth Michael ndiyo maana wakati ananirudisha tayari bahasha ilikuwa imefunguliwa.”
Barua ya uchumba iliyowasilishwa na mshenga kwa mama Lulu.
UTARATIBU ULIFUATWA?
Risasi lilimuuliza mshenga huyo kama bosi wake alifuata utaratibu wa barua za posa katika utamaduni wa Kitanzania ambapo ndani ya bahasha huwekwa pesa kidogo.“Tulifuata utaratibu wote, ndani ya bahasha tuliweka shilingi laki moja na zimerudi zote.”
MAMA LULU ANASEMAJE?
Baada ya kudokezwa ishu hiyo, Risasi lilimtafuta mama mzazi wa Lulu ili kumsikia anasemaje kuhusu madai ya mshenga huyo, kwamba alipeleka kweli barua ya posa kwa Lulu au alikwenda kwa shida nyingine.
“Mimi mwenyewe nawashangaa ninyi waandishi. Mambo ya kuolewa anayetakiwa kuulizwa ni Lulu mwenyewe. Kama mtu alileta barua au nini, Lulu ndiyo atajibu.
Staa ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Halafu naomba kuwaambia kwamba nilishasema siku nyingi mimi sitaki mambo ya magazeti, hata hao mabosi wenu niliwahi kuwaambia,” alisema mama Lulu na kukata simu.
LULU HAPOKEI SIMU
Baada ya kuzungumza na mama mtu, gazeti hili lilimsaka Lulu mwenyewe ili kumsikia anazungumziaje kuhusu barua hiyo lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.