MIZINGUO! Mbongo Fleva aliyewahi kutamba na wimbo wa Jela, Hussein Machozi amefunguka kuwa tuhuma za kumtelekeza mke wake Shuena Yunus Omar, Mombasa Kenya hazimtesi kwa kuwa alioa kama geresha tu.
Machozi alifunguka hayo Januari 16, mwaka huu, alipobanwa na paparazi wetu azungumzie ukweli wa sakata la kudaiwa kumkimbia mkewe huyo lililotapakaa kama moto wa kifuu kwenye mitandao ya kijamii.
Mbongo Fleva aliyewahi kutamba na wimbo wa Jela, Hussein Machozi akiwa na mke wake, Shuena Yunus Omar kabla ya kumkimbia.
Machozi alisema anashangaa kusikia watu wanakomalia ishu hiyo wakati yeye alimuoa mwanamke huyo kama geresha ili aweze kuishi nchini humo kwa amani lakini hakuwa na nia ya dhati ya kuwa na mwanamke huyo.
Mtoto wa Mombasa, Shuena Yunus Omar akitabasamu.
“Kweli kaka Mombasa nilikuwa na mke lakini mazingira ya kuoa kwangu yalipelekewa na ugumu wa kuishi nchini humo, hivyo nikaamua kuingia kwenye ndoa hiyo kwa geresha, si unajua kuishi nchi isiyokuwa yako lazima uwe mjanja sana la sivyo kutimuliwa kunakuwaga njenje.
Hussein Machozi akipozi kimahaba na mkewe huyo kitandani.
“Najua ni kweli mwenzangu alikuwa na mapenzi ya dhati kwa asilimia mia moja ila mimi nilikuwa na lengo langu kichwani, hivyo nimemwacha na kurudi home. Haya yaliyotokea mimi hayaniogopeshi kwani sijamfanyia ukatili wowote wala sijampa ujauzito kwamba atateseka na mtoto,” alisema Machozi.