Monday, January 5, 2015

MASAJU AAPISHWA KUWA MWANASHERIA MKUU


Mwanasheria Mkuu Mpya wa Serikali Mhe. George Masaju amewaomba Watanzania wajenge imani na serikali yao huku akiahidi kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mheshimiwa Masaju amesema hayo leo muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Tanzania Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo uliokuwa ukishikiliwa na Jaji Frederick Werema ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi wa Escrow.

Kwa mujibu wa Masaju, maeneo ambayo atayaangalia ni pamoja na suala na kilio cha muda mrefu cha wanachi na wabunge la kutaka uwazi katika mikataba mbalimbali ambayo serikali imekuwa akiisaini kwa niaba ya wananchi.