Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema baada ya watu hao kufanya unyama huo, waliuweka mwili wa mtoto huyo katika sinki la kuogea kwenye nyumba moja ambayo haijakamilika ujenzi wake. Pamoja na hayo, alisema upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.
Akizungumza eneo la tukio, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.
Akizungumza eneo la tukio na paparazi huru, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.
"Nilipota taarifa hiyo, niliongozana na majirani tukiwa na ndugu wa marehemu na kushuhudia mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa kwenye sinki la kuogea huku sehemu zake za siri zikiwa zimeharibiwa vibaya"
Mama mlezi wa mtoto huyo, Sala Mwandobo, alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani kwake January 7 mwaka huu baada ya kuaga anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji lililopo mbali kidogo na nyumbani kwake.