Friday, January 2, 2015

"MBALI YA KUNIZAA KWA UCHUNGU, ULIZIBEBA AIBU ZANGU"...UJUMBE MZITO WA LULU MICHAEL KWA MAMA YAKE

“Huwezi kuamini Ilinibidi nianze kuandika hii risala 3day before ur birthday (mana Sio caption tena)
 
Kwanza nashukuru kwa MAPENZI na heshima uliyonipa kwa kuniweka tumboni kwako miezi 9,kunizaa kwa uchungu na kunilea kiroho,kiakili na ki mwili pia...Namshukuru Mungu kwa kunipa ww kama Mzazi WANGU na ninajivunia hilo sana..!
 
Kuna wakati nakukosea na kukuumiza Lkn kiukweli huwa naumia na kujuta sana baada Ya kujua kosa langu.
 
Licha Ya uchungu uliopata kwa kunizaa na kunilea upo wakati nilipitia mambo yaliyozidi kukuumiza zaidi Ya uchungu wa kunizaa ila ktk yote ulisimama na ulizibeba Aibu zangu bila kujali jamii,familia au watu binafsi wange kuchukuliaje,Naamini wewe pekeyako ndio mtu pekee ninayeweza kusimama kwa kujiamini na Kusema ni WANGU Pekeyangu.
 
Una mapenzi Ya kweli,naamini Hata kama kuna wazuri wenye akili,wenye maumbo,muonekano au wenye kitu chochote kilicho bora Zaidi yangu bdo kwenye macho na Moyo wako utaniona Mimi ni bora zaidi Ya yoyote Duniani.
 
 Nakuombea Afya,Uzima,Furaha,Mafanikio na kutimizwa kwa haja zote za moyo wako.Ninakujua kama mama bora,mwanamke jasiri,mwenye msimamo,busara,hekima,mcheshi na rafiki....NENO NAKUPENDA tu halitoshi

HAPPY BIRTHDAY THE QUEEN OF MY HEART
HAPPY BIRTHDAY MAMA
Risala itaendelea nyumbani kwa Dada wa Rwechungura mana ntakesha hapa". Lulu alimaliza.

 
Bandiko hili aliliweka usiku wa kuamkia jana.