Rais Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amewaongoza Wananchi wa Zanzibar katika maandhimisho ya Miaka 51 ya Mapinduzi na kutangaza kuwa kuanzia mwaka huu, Elimu ya Awali na Msingi itatolewa bure kwa kuwa serikali itagharamia gharama zote na pia kwa Elimu ya Sekondari, serikali itagharamia ada ya mitihani ya kuhitimu kidato cha 4 na kidato cha 6.