MKIA wa Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea na watu 162 Desemba 28, mwaka jana umepatikana leo katika Bahari ya Java, Indonesia.
Eneo la mkia ndipo kifaa cha kutunza kumbukumbu za ndege 'black box' kinapatikana na upatakianaji wake utasaidia wachunguzi kubaini chanzo cha ndege hiyo kupotea na kisha kuanguka baharini.
Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Jiji la Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singaporea. Mpaka sasa miili 40 imeopolewa kutoka baharini katika eneo ambalo ndege hiyo ilianguka.