Thursday, January 29, 2015

“NADHANI AVEVA HANA CHA KUSEMA NA WALA ASITHUBUTU AONANE NA UKAWA NA KUFANYA SIMBA IWE MOJA”

aveva
Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva
Na Agnatius Obel
HUKO Ujerumani kuna timu inafanya vibaya kuliko Simba, ni Borrusia Dortmund, ni ya pili kutoka mwisho, lakini bado wana Kocha yule yule waliyeanza naye msimu!
Hapa kwetu Simba imeshafukuza Kocha mmoja, na bado matokeo ni mabaya na kuna uwezekano yakaendelea kuwa mabaya!
Tofauti iliyopo kati ya Simba na Borrusia ni: nani anaamini nini?
Kwa Borrusia washabiki na hata wadau wanaamini ni kipindi cha mpito japo nao wanaweza kufukuza Kocha, lakini hapa kwetu ni mwiko kuwa na kipindi cha mpito au kusema mambo ya mpira, ni lazima Simba ishinde na kukaa juu!!
Kiukweli popote pale, kama timu haifanyi vizuri lazima Kocha atawajibika na kuangalia mambo mengine, lakini pia si kila wakati timu inapofanya vibaya basi ni tatizo la Kocha!
Hakuna tasnia ninayoichukia kama ya habari hasa za michezo hapa Tanzania, hakuna weledi, wanahongwa, hawafanyi utafiti kwa kina, ni watu wa kupelekwa pelekwa tu!
Hakika wanaiharibu jamii sio siri, inakubidi uwe makini sana ili usiingie kwenye mkumbo wa kuhadaika!!
IMG_6078 (2)
Nina maana kusema hivi, ni kweli Simba ina matatizo, ukiwa unaujua mpira ukiiangalia tu Simba unajua ina mapungufu, lakini pia hata mpira wa hapa una mapungufu tena mengi tu, kwa hiyo pamoja na mapungufu ya Simba bado inaweza kufanya vizuri!!
Waandishi wa habari, kama kuna mtu walikuwa wanamsakama kila kukicha, basi alikuwa Rage, japo cha kushangaza hakuwahi kuwa kwenye mwenendo mbaya kama huu!!
Waandishi wa habari, wanaiaminisha jamii kwamba ‘Friends of Simba’ ndio kila kitu Simba………je wameshafanya uchunguzi wa kutosha kwenye hili??
Basi hata washabiki wa Simba nao wanaamini hivyo, na kibaya zaidi wamefungwa likishindikana kwa ‘Friends of Simba’ ndio basi tena!!
Kwa mtu yoyote anayeangalia mpira kwa umakini na kuufahamu pia, Simba wana matatizo ya, Golikipa mahiri, beki wa kati, kiungo mshambuliaji na mshambuliaji!!
Mpira kila mtu ana jinsi anavyoutazama, siwezi kuelezea kwa mapana sana kwanini nazungumzia hizo nafasi, lakini wanasema mpira ni mchezo wa wazi hakuna cha kujificha!
Kwenye timu lazima uwe na wachezaji wasiopungua watano ambao ni ‘outstanding perfomer’ hata kama siku wanakuwa wako vibaya basi wenzao wanawabeba!!
Niseme tu, ni Mkude pekee ndiye mchezaji mahiri na anaweza kucheza na watu wa aina yoyote kwa sasa, wachezaji wengine wanapanda na kushuka, kitu ambacho kwenye timu iliyopo kwenye ligi ni majanga!!
Tatizo la Tanzania ni kutofautisha ni aina gani ya wachezaji wanaofaa kushindana na kuleta mafanikio na wachezaji wenye uwezo kupiga chenga
na visigino, Simba kuna wachezaji wengi sana katika suala la kuchezea mpira ni mahodari,  lakini je wanaisaidia timu ipasavyo kwenye ligi??
Simba ya Aveva imemruhusu Tambwe aondoke kwa sababu wanazojua wao, lakini si za kisoka naamini, bado walimwacha comanding center back Musoti kwa ajili ya Okwi, sio mbaya.
Okwi ni mzuri halina ubishi lakini ndio tumkate Musoti bila kuwa na mbadala wake?? Ikumbukwe Kaze Gilbert alishindwa kucheza na Owino kwa sababu ya aina zao kulingana, ni kama Hassan Isihaka na Juuko na Owino pia ambaye ni kama ameonyeshwa mlango wa kutokea, lazima apatikane mtu mgumu mmoja!!
Lakini waandishi wa habari hawaichambui Simba kama walivyokuwa wakifanya wakati wa Rage, ni kwa kuwa wanaamini Friends of Simba ni kila kitu, lakini kama pia walikuwa wakihongwa ili wamchafue
Rage ili aonekane hafai na leo wanaomhonga wako madarakani, unafikiri watafanyaje??
Sipati picha kama Rage angekuwa madarakani, ni mara ngapi ungewasikia wale wale, tuachie timu yetu, lakini leo sio kwamba hawapo wapo ila kwa kuwa Friends ndio kila kitu basi hewala!!
Uongozi ni busara pia, sitaki kuamini sana mambo ya Ukawa, lakini kwa utamaduni wa mpira wetu mambo ya nje nayo si ya kudharau, lakini tumefikaje hapa??
Kwani mbona watu wa Friends wameshawahi kuongoza na bado Simba ikawa moja, kwanini  sasa iko tofauti??
Friends wana uzuri na athari zake, Aveva kama mtawala mzuri, kuna mambo nina uhakika hata yeye hakupenda yatokee lakini kwa nguvu aliyowapa Friends mambo yamemzidi, hakuja asiyejua kama Phiri ilikuwa kama kafara tu, na hata Aveva mwenyewe imenukuliwa hakujua kama Phiri alifutwa kazi wakati muafaka zaidi ya kupewa taarifa tu!!
Nadhani Aveva hana cha kusema na wala asithubutu aonane na Ukawa na kufanya Simba iwe moja!!
Sifurahii Ukawa hata kidogo, lakini narudia tena nawachukia waandishi wa habari, Simba imekuwa ikiumizwa sana na Friends of Simba na kuhujumiwa pia pindi Uongozi unaokuwa madarakani hawaelewani, sasa imegeuka na wao wanaionja joto ya jiwe, nadhani ndio maana walijiamini kwamba wao wako madarakani basi kila kitu sawa, lakini wamesahau hizi timu zina wenyewe!
-shaffih dauda